Bonyeza Kujiunga nasi WhatsApp Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.
Nafasi za Ajira Afisa Ukuzaji Viumbe Kwenye Maji Msaidizi Daraja la II MDAs & LGAs
| Kigezo | Maelezo |
|---|---|
| Nafasi | Afisa Ukuzaji Viumbe Kwenye Maji Msaidizi Daraja la II |
| Mwajiri | MDAs & LGAs |
| Idadi ya Nafasi | 1 |
| Muda wa Maombi | 15/10/2025 – 30/10/2025 |
Majukumu
Kuhamasisha kuongeza ubora wa mazao na ukuzaji viumbe kwenye maji ili kulinda soko na afya ya walaji.
Kuwaelimisha wananchi juu ya ufugaji wa samaki, kilimo cha mwani, na usimamizi endelevu ili kuongeza tija.
Kuanisha wawekezaji katika shughuli za ukuzaji viumbe kwenye maji na kuhamasisha uwekezaji huo.
Kuhakiki ubora na usafi wa zana za kuvunia mazao ya viumbe wa majini, maeneo ya kuhifadhi na usafirishaji wake.
Kusimamia maandalizi ya mashamba darasa ya ukuzaji viumbe kwenye maji.
Kutekeleza majukumu mengine ya fani yake atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
Sifa za Mwombaji
Awe mhitimu wa Kidato cha IV au VI mwenye Stashahada (Diploma NTA Level 6) ya ukuzaji viumbe kwenye maji kutoka Chuo cha Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) au sifa inayolingana kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320,
Mtaa wa Mahakama, Tambukareli,
DODOMA.