Bonyeza Kujiunga nasi WhatsApp Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.
Nafasi za Ajira 224 Afisa Hesabu Daraja la II MDAs & LGAs
| Kigezo | Maelezo |
|---|---|
| Kazi | Afisa Hesabu Daraja la II |
| Mwajiri | MDAs & LGAs |
| Idadi ya Nafasi | 224 |
| Muda wa Maombi | 15/10/2025 – 30/10/2025 |
Majukumu:
Kushiriki kuandaa taarifa za mapato na matumizi.
Kushiriki kuandaa taarifa za maduhuli.
Kushiriki kufanya usuluhisho wa hesabu za benki na nyingine zinazohusiana na masuala ya fedha.
Kuandaa taarifa mbalimbali za mishahara.
Kuandika hati za malipo na hati za mapokezi.
Kutunza daftari za amana.
Kutekeleza kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
Sifa za Mwombaji:
Awe na Cheti cha Kati cha Uhasibu Intermediate Certificate (Module D) kinachotolewa na NBAA au sifa nyingine zinazolingana zinazotambuliwa na NBAA.
Awe pia na Shahada ya Biashara au Sanaa aliyejiimarisha katika fani ya Uhasibu, au Stashahada ya Juu ya Uhasibu kutoka Taasisi inayotambuliwa na Serikali.
Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320,
Mtaa wa Mahakama, Tambukareli,
DODOMA.