Ajira 131 Mhasibu Daraja la II

Bonyeza Kujiunga nasi WhatsApp Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Nafasi za Ajira 131 Mhasibu Daraja la II MDAs & LGAs

KigezoMaelezo
KaziMhasibu Daraja la II
MwajiriMDAs & LGAs
Idadi ya Nafasi131

Muda wa Maombi: 15/10/2025 hadi 30/10/2025

Majukumu
Kuandika taarifa za mapato na matumizi.
Kuandaa taarifa za maduhuli.
Kupokea maduhuli ya Serikali na kuhakikisha yanawekwa Benki kwa wakati.
Kufanya usuluhisho wa akaunti za Benki na akaunti nyingine zinazohusiana na masuala ya fedha.
Kukagua hati za malipo.
Kutekeleza majukumu mengine ya taaluma yake atakayopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

Sifa za Mwombaji
Awe ni mhitimu wa Kidato cha Sita mwenye Shahada ya Uhasibu au Biashara aliyejiimarisha katika fani ya Uhasibu, au mwenye Stashahada ya Juu ya Uhasibu kutoka Taasisi inayotambuliwa na Serikali.
Awe pia na Cheti cha Taaluma ya Uhasibu CPA (T) au sifa inayolingana inayotambuliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA).

Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;

KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320,
Mtaa wa Mahakama, Tambukareli,
DODOMA.

Tuma maombi hapa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.