Ajira 24 Mhandisi Kilimo Daraja la II

Bonyeza Kujiunga nasi WhatsApp Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Nafasi za Ajira 24 Mhandisi Kilimo Daraja la II MDAs & LGAs

KigezoMaelezo
KaziMhandisi Kilimo Daraja la II
MwajiriMDAs & LGAs
Idadi ya Nafasi24
Muda wa Maombi15/10/2025 – 30/10/2025

Majukumu:

Kuandaa programu za mafunzo kwa wakulima juu ya matumizi ya zana za kilimo.
Kushiriki katika kutoa mafunzo kwa wakulima kuhusu matumizi bora ya zana za kilimo.
Kushiriki kutengeneza michoro na ramani za miradi ya umwagiliaji.
Kushiriki katika ujenzi wa miradi ya umwagiliaji.
Kushirikiana na mafundi sanifu kuwafundisha wakulima uendeshaji wa skimu za umwagiliaji.
Kukusanya takwimu za miradi ya umwagiliaji.
Kushiriki kuratibu na kutoa huduma za umwagiliaji kwa vikundi vya wakulima pamoja na matumizi ya maji.
Kuandaa mafunzo na maonyesho kuhusu matumizi ya zana za kilimo.
Kufuatilia programu za mafunzo kwa wanyama kazi, mafundi wa matrekta na wakulima juu ya matumizi ya wanyama na matrekta.
Kuwafundisha wakulima ujenzi wa vihenge bora vya kuhifadhia mazao.
Kushughulikia ubora wa zana za kilimo na kutoa ushauri kwa waagizaji na watengenezaji.

Sifa za Mwombaji:

Awe na Shahada ya Kwanza (Bachelor Degree) ya Uhandisi yenye mwelekeo mkubwa katika fani ya Kilimo cha Umwagiliaji au Zana za Kilimo kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali.

Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;

KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320,
Mtaa wa Mahakama, Tambukareli,
DODOMA.

Tuma maombi hapa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.