Bonyeza Kujiunga nasi WhatsApp Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.
Nafasi za Ajira 32 Afisa Tawala Daraja la II MDAs & LGAs
| Kigezo | Maelezo |
|---|---|
| Kazi | Afisa Tawala Daraja la II |
| Mwajiri | MDAs & LGAs |
| Idadi ya Nafasi | 32 |
| Muda wa Maombi | 15/10/2025 – 30/10/2025 |
Majukumu:
Kutoa mapendekezo kuhusu utekelezaji wa Sheria, Sera, Kanuni na Taratibu mbalimbali zinazotolewa na Serikali.
Kutoa mapendekezo kuhusu kazi za utawala na uendeshaji katika Ofisi za Serikali.
Kushughulikia masuala ya itifaki mahali pa kazi.
Kuweka kumbukumbu za matukio muhimu ya taasisi.
Kupokea na kusajili malalamiko mbalimbali yanayowasilishwa.
Kusimamia miundombinu ya Ofisi na Majengo.
Kushiriki katika maandalizi ya vikao vya Baraza la Wafanyakazi.
Kushughulikia masuala ya anuai za jamii.
Kuratibu shughuli za maafa.
Kutekeleza kazi nyingine za kada yake kama atakavyoelekezwa na msimamizi wa kazi.
Sifa za Mwombaji:
Awe na Shahada katika mojawapo ya fani zifuatazo: Public Administration, Political Science and Public Administration, Business Administration au Commerce iliyojiimarisha katika Human Resources Management, Leadership and Governance, Public Administration and Management, Local Government and Management, Human Resource Planning and Management, Human Resources Management, Human Resources Planning, Labour Relations and Public Management, Industrial Relations, au fani nyingine zinazofanana kutoka Taasisi au Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320,
Mtaa wa Mahakama, Tambukareli,
DODOMA.